Wadau wa jiko letu, leo tuna visheti. Visheti ni aina ya kitafunwa, chaweza liwa na kahawa, chai, juisi na hata maji . Ila kwa chai na kahawa vinapendeza zaidi. Kuna namna tofauti tofauti za uandaaji wa visheti, kukandia nazi, mara nyengine mafuta, waweza pia kukandia siagi na hata maziwa. Vya leo tutatumia siagi, na tukijaaliwa siku nyengine tutapika na hizo aina nyengine.
Mahitaji ya Kuandaa Visheti
Ngano kilo1
mafuta lita1
siagi robo kilo
yai 1
Hiliki kiasi
baking powder kijiko1
Chumvi kidogo sana
Sukari nusu
JINSI YA KUPIKA Visheti
Chunga unga wako, weka baking powder, tia chumvi kidogo ukipenda, tia sukari kidogo na hiliki changanya na siagi uvurugetia mafuta nusu kikombe, endelea kuvuruga unga wakopiga yai litie kwenye unga, endelea kuvurugaongeza maji kiasi ili unga wetu uweze kukandika na kushikana kuwa donge moja.
Tengeneza vidonge vidonge, kisha uviviringishe hadi viwe kama fimbo, baadae weka kwenye kibao ukatekate visheti vidogo dogo
Weka mafuta kwenye karai jikoni, yakipata moto kaanga visheti hadi viive, kisha vitoe pembeni uanze kuandaa SHIRA
Andaa shira kwa kutumia sukari nusu, na maji kikombe cha chupa ya chai kimoja, bandika jikoni maji ulotia sukari yachemke hadi yatoe povu na ukiitoa kidogo ukiishika inanata sana, hapo shira ni tayarimimina visheti ulokaanga kwenye sufuria ya shira, weka na hiliki, kisha vipetepete ili vijigeuze na kuenea sukari vyote. Vikiwa tayari vimekaukia sukari vizuri, visheti vyetu weka kwenye chombo tayari kumfikia mlaji
Visheti vyetu tayari wadau, mimi huvipenda hivi vya kukandia siagi sababu hukaa muda mrefu bila kuwa vigumu. Kwa hiyo waweza tengeneza ukala na vikibaki unavihifadhi vizuri kwa ajili ya kutafuna siku nyengine.
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.