Vipimo
Unga – 2 gilasi
Siagi – 1 pound
Sukari – 1 pound
Mayai – 10 – 12
Baking powder – 1 kijiko cha supu
Vanila – kiasi
Rangi mbali mbali
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Keki ya Rangi Rangi
Washa oveni moto wa kiasi 350 degrees.
Weka siagi na sukari katika mashine ya keki, saga mpaka iwe laini.
Tia mayai uchanganye kwa speed ndogo. Tia vanilla changanya vizuri.Tia unga uliochanganywa na baking powder changanya vizuriChota unga kidogo kidogo weka katika vibakuli mbali mbali utie vitone vya rangi mbali mbaliKisha changanya pamoja na mchanganyiko uliobakia, chukua kisu cha siagi uchanganye kufanya rainbow.Paka siagi katika treya ya kupikia keki.Mimina mchanganyiko upike kiasi ya nusu saa.Epua, subiri ipoe ukate upendavyo ikiwa tayari