Home Mapishi Jinsi ya Kutengeneza Swiss rolls

Jinsi ya Kutengeneza Swiss rolls

by komzinski
swiss rolls - malindi kenya recipe

Swiss rolls, ama roll cake, jelly au Swiss log is aina fulani ya cheki zinazojulikana kama sponge cake ambazo hujazwa jam, icing au whipped creamed. Licha ya kuwa na jina “Swiss”, kuashiria kutoka nchi ya Uswizi (Switzerland), inaaminika kuwa asili yake in Uropa ya kati haswa nchi ya Austria.

Waswahili nao wako na mitindo yao ya kutengeneza swill rolls. Watu wa Malindi, wakiwemo, wamekuwa wakitumia mitindo hio huku wakichanganya na mitindo asilia kutoka uropa kutengeneza vyakula hivi.

Aina za Swiss rolls

 

Mahitaji ya kutengeneza Swiss Rolls (cake rolls)

Mayai 3
Sukari nusu kikombe
Kijiko kimoja arki ya vanilla
Chumvi robo kijiko cha chai
Unga nusu kikombe
Baking powder nusu kijiko cha chai
Jam ya strawberry vijiko 6 vya kulia au chocolate hazelnut spead

Namna ya kutengeneza swiss rolls

Tenganisha mayai ute mbali na viini mbali piga ute na sukari mpaka iwe nyeupe iwe ukilipindua Bakuli haimwagiki tia viini vya mayai, tia arki vanilla, tia baking powder na mwisho malizia kutia Unga ukimaliza tia kwenye tray uliyoifunika na ile wax paper uipake mafuta au samli au siagi. Tia mchanganyiko wako ndani ya tray choma kwa dakika 10-12. Ikiwa tayari itowe kwenye tray itowe ile wax paper uliyoibake nayo kata wax paper nyengine iweke na juu yake iweke ile cake yako ipake jam halafu iroll kama inavyoonyesha kwenye picha.

swiss rolls

NB:- Aina hii ya cake huwa haiwekwi siagi/butter/blueband wala mafuta na inakuwa soft na laini sana kuliko cake ya kawaida.(kama ilivyo mkate wa mayai)
-wakati wa kuoka hakikisha unatumia tray pana au kama unapikia jiko la mkaa basi utumie chombo kipana ili ipate kuenea vizuri iwe nyembamba/flat na baadae uweze kuikunja bila ya tabu.
-wakati wa kukunja unatakiwa ukunje taratibu kwa umakini ili cake isiharibike au kukatika
-hapo kwenye kupaka kama huna jam unaweza kutumia chocolate, icing sugar, cream n.k

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More

Privacy & Cookies Policy