Jinsi ya kutengeneza Mahamri ya kusuka la maziwa
Mahitaji
Unga ngano nusu kilo
Maziwa robo
Sukari nusu kikombe
Maziwa robo lita
Hamira kijiko kimoja kidogo
Samli vijiko viwili
Iliki robo kijiko kidogo iloyosagwa
Mafuta ya uto kijiko kimoja kidogo
Namna ya kupika
- Unga na samli wauchanganya hadi uchanganyike vizuri kisha weka iliki yako
- Tia hamira pamoja na maziwa, kanda mpaka unga ulainike
- Kisha gawanya mara tatu, sokota zote tatu alafu zote tatu wafanya kama kuzisonga.
- Ukishamaliza wachukua sufuria yako safi, wapaka mafuta yako kwa wembamba.
- Wemba unga uliokandwa kwenye sufuria , oka kwa muda wa takriban dakika ishirini.
- Andaa kwa chai ya maziwa
Hamri la kusuka la maziwa
Namna ya kupika
-
Unga na samli wauchanganya hadi uchanganyike vizuri
-
kisha weka iliki yako
-
Kisha gawanya mara tatu, sokota zote tatu alafu zote tatu wafanya kama kuzisonga.
-
Ukishamaliza wachukua sufuria yako safi, wapaka mafuta yako kwa wembamba.
-
Wemba unga uliokandwa kwenye sufuria , oka kwa muda wa takriban dakika ishirini.
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.