Mahitaji ya kutengeneza keki ya nanasi
Nanasi vipande 6
Yai moja
Maziwa kikombe kasoro
Chumvi nusu kijiko kidogo
Siagi thuluthi kikombe
Sukari kikombe kimoja
Namna ya Kutayarisha keki ya nanasi
Kwanza tayarisha shira ama mraba kwa kutumia maji na vijiko 6 vya sukari, pika kama vile sukari ya pudini
Washa oven kwa moto wa 180
Chukuwa baking slide zako za nanasi zipange vizuri kisha mimina shira yako juu tandaza vizuri.
Sasa tayarisha urojo wako wa keki, chukuwa bakuli lako weka yai, maziwa, chumvi, baking powder pamoja na siagi yako, sukari sasa piga tena.
Baada ya mchanganyiko kukoregeka vizuri mimina mchanganyiko wako juu ya baking pan yako juu ya ile nanasi pamoja na shira.
Weka kwa oven yako kwa moto wa 180 kwa muda wa dakika 45 ama 50.
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.