Mahitaji
Kamba (Prawns) 500g
Pilipili manga (Black Pepper) ½ kijiko kikubwa
Kitunguu swaumu 1
Limau 1
Chumvi kijiko kidogo cha chai
Curry powder kijiko 1 kikubwa
Nyanya 3 (au nyanya za kusaga za kopo)
Haradali (Mustard) vijiko 3. (Hii ni maalum kuondoa harufu ya shombo kwenye kamba)
Kupika
Kuandaa kamba
Ondoa magamba kwenye kamba kama bado wana magamba
Osha kamba kwa kusuuza na maji kiasi.
Kamulia limao kwenye kamba, changanya kiasi na kisha ongeza chumvi. Acha kwa muda wa dakika 3, halafu weka hao kamba kwenye chujio ili kuchuja maji na kuacha kama wakavu tayari kwa kupikwa.
Bandika kikaango kwenye jiko. Acha ipate moto kiasi, kisha ongeza mafuta ya kula kama ¼ lita (pima kutokana na wingi na ukubwa wa kamba ulionao). Acha yapate moto kwa muda.
Ongeza kamba wako kwenye mafuta. Acha waive hadi wabadilike rangi kuanza kuwa wa brauni. Geuza geuza ili waive pande zote.
Ongeza haradali kwenye kamba, koroga taratiibu hadi ichanganyike vizuri.
Wakishaiva, toa kamba.
Kuandaa mchuzi wa nyanya
Ili kuleta ladha kwenye chakula, andaa mchuzi kiasi wa nyanya ili kuchanganya na kamba.
Kuandaa tambi
Bandika maji kiasi kwenye sufuria, weka chumvi kisha ongeza tambi.
Acha mchanganyiko uchemke kwa muda wa dakika 5 hadi 6. (Angalizo: Tambi huiva chini ya dakika 10, ila itakuwa vizuri kama utatoa wakati bado ngumu ili zisipondeke wakati wa kupika na kamba.)
Chuja maji kwenye tambi kwa kutumia chujio.
Kuchanganya
Changanya Tambi kwenye mchuzi wa nyanya. Koroga hadi mchanganyiko uwe vizuri.
Changanya kamba kwenye mchanganyiko wa tambi na nyanya. Koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 3.
Ongeza Curry powder na kitunguu swaumu kilichosagwa kwenye mchanganyiko, koroga kiasi.
Ongeza pilipili manga kwenye mchanganyiko. Koroga ili kupata mchanganyiko zaidi.
Acha mchanganyiko uchemke kwa dakika 2 kisha ipua na unaweza kula.
Furahia.
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.