Mapishi ya Juice

Juisi ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na kukamuliwa au kubanwa kwa kioevu asilia kilichomo kwenye matunda.

Matunda yaliyo maaarufu katika kutengenezaji wa juisi ni kama: ovacado, maembe, machungwa, tikiti maji, karoti , tufaha na vinginevyo.

Katika mapishi ya juice kuna mitindo tofauti inayotumika, hii inajumuisha kubana au kuchanganya.

Juisi za ovacado, tikiti maji, karot, maembe huchanganywa kutumia kifaa kinachojulikana kama blender, halikadhalika juisi ya machungwa na ndimu hukamuliwa kutumia sqmapishi ya juiceueezer.

Faida za Kiafya za Juisi Iliyokamuliwa au kutengenezwa nyumbani

Juisi safi zimejaa fiber ambayo ni nyuzi mumunyifu, aina ya nyuzi zinazosaidia ukuaji mzuri wa bakteria na afya ya usagaji wa chakula.

Juisi zilizopuliwa upya huupa mwili wako kiasi kikubwa cha maji. Maji haya hufanya kazi ili kusaidia mwili kusindika wanga, ambayo hutoka kwa sukari asilia kwenye juisi, pamoja na vitamini, madini na viitamini kutoka kwa chanzo kizima cha chakula.

Jusi huupa mwili sukari asilia na hakuna vihifadhi. Juisi nyingi zilizowekwa tayari zimetengenezwa kwa vihifadhi ambavyo huondoa thamani ya lishe.

Juisi zisizo za kawaida

Kuna aina ya juisi ambazo si za kawaida, yaani ambazo haziko maarufu haswa katika migahawa lakini huwa na faida kuu katika afya ya mwanadamu. Juisi ya beti, karoti na tomato ni mifaano ya juisi hizi.

Maziwa pia hutumika katika utengenezaji wa juisi kama za ndizi na vinywaji vingine almaarufu milkshake.

Juisi Mjini Malindi

Malindi ukiwa kati ya miji wenye joto jingi nchini Kenya, kinywaji hua cha thamani, haswa kikiwa kimepozwa.

Mji huu unaojulikana kwa utalii wa kimataifa na kitaifa umejaa maeneo kama migahawa na hoteli ambazo zina juisi kwa wingi.

Utamu wa juisi Malindi

Ili kufurahia juisi hizi mjini malindi, kaunti ya Kilifi; tembelea Jameel Dishes Malindi na Seafront Dishes kupata ladha tofauti za juisi hizo.

 

 

 

 

 

 

 

Follow Along

New guides, local stories, and coastal updates — posted first on social.