Connect with us

PEOPLE OF MALINDI

Nelly Boy

Published

on

Nelly Boy

Kwa majina kamili ni Nelson Randu lakini jina La stage anajulikana Nelly boy. Jina Nelly lilitokana na ufupisho wa jina Nelson. Anafanya mziki ambao umekuwa chanzo kikubwa kukua kisanii kwani huwa anahisi umekuwa ukimjenga sana hasa katika utunzi wake wa mashairi.

Nelly Boy kama kioo cha Jamii

Amekuwa akitunga mashairi na kuimba kuhusu matukio yanaomtokea maishani; yaani vitu ambavyo ni true story. Kama kioo cha jamii Nelly boy anazungumzia masuala ambao hukumba jamii kwa njia moja ama nyengine. Mashairi yake au mtindo wake wa sanaa anavyodai Nelly boy ni mziki wa hisia. Amefananisha mtindo wake kama ule wa Harmonize, Mbosso, Aslay, Ally Mahaba. Mtindo wa mziki wa wasanii  humjenga sana kiutunzi na ana imani kuwa  atafika walipo siku moja. Nitazidi kujituma na hata zaidi kufikia malengo na kukamilisha ndoto zangu.

samahani release pilkapilka nelly boy - Nelly Boy

Masomo yake Nelly Boy

Alisomea shule ya Msingi Garashi, ilioko eneo mbunge la Magarini katika sehemu ya zamani ya Wilaya ya Malindi.  Alihitimisha masomo yae mwaka wa 2009 na bila ya kuchelewa alijitosa katika hali za kujitaftia maisha.

Baada ya “Kuhustle” kwa kipindi cha miaka mitatu vile, alianza safari yake ya mziki. Mwaka huo wa 2012 ulimuona akifanya kazi zake za sanaa katika studio mmoja mjini Malindi, Terabyte Records,  iliyomilikiwa na producer Jokka ambaye pia anajulikana kama Ndale Ndale. Japo mambo yake hayakuenda vizuri lakini hakukata tamaa ila ilimlazimu kusitisha kidogo kazi zake za mziki kwa sababu ya ukosefu wa fedha kwa kipindi cha miaka sita.

Mwaka wa 2018 uliona ujio wake mpya katika sanaa. Alirudi rasmi kwa game na kuanza kufanya kazi zake katika studio za MK2 Studios chini ya producer Magustu Babu. Ujio huu ulifanya nyota yake kuanza kung’aa hasa pale alipofanya kibao Maumivu kilicho mpa nafasi ya kujulikana na mashabiki wake.

READ  Asfat AbdulRazaq

Mafanikio ya Nelly Boy

Kibao cha Maumivu kimemfanya Nelly Boy ajivunie alipofikia kwa sasa. Juhudi zake zinampa furaha na matumaini kwani anaona akisonga mbele kila kunapokucha. Cha mno ni kurejesha shukurani mashabiki wake na kusisitiza mapenzi yake kwao na kuwaomba waendeleee kumpatia support zaidi na ameweka ahadi ya kutawaangusha kamwe. Anasema anawaandalia mazuri zaidi na watakubali hata zaidi sana.

“Yeah ata sikua nafikiria kama ni talent cs nlikua napenda sana kujiunga na tamasha ata shuleni but nilikua nachukulia tu kama mchezo wa kujifurahisha cs hata nlikua nikitunga mashairi amabayo hata waalimu walikua wananikubali but sikua najua kama no safari ya mziki nimeanza.
Na nlikua Mara nyingi nikiwa kwa barabara naeza pata idea tu ya ngoma naimba nikitembea naeza imba kama ngoma tatu lakini sikua naeza zinakili nikidhani najifurahisha tu”

Kwa sasa matunda yenyewe bado Ila mda sio mrefu mavuno nitayafurahia kwa sababu mashabiki wangu wamenipa moyo na nimepiga hatua zaidi kitu ambacho nakifurahia kwa sasa.

Kazi zake Nelly Boy

Kwa sasa hivi ameweza kutunga na kurekodi nyimbo sita. Kati ya hizi ni ngoma moja pekee ambayo ameweza kuifanyia video, Maumivu. Nelly Boy ako katika utaratibu wa kutengeneza video nyengine ambayo ipo njiani mda wowote itakua inakamilika.

1.Maumivu
2.Muda
3.Samahani
4.Hukutaka
5.Niambie
6.Chuki.
Ameweza kufanya kazi mbili akiwashirikisha wasanii wengine kama vile Sollobizzo na Shaa Biggy na vile vile ni kazi ambazo amefanya na studio mbali mbali na ma produza tofauti.

We endeavor to keep our content True, Accurate, Correct, Original and Up to Date.If you believe that any information in this article is Incorrect, Incomplete, Plagiarised, violates your Copyright right or you want to propose an update, please send us an email to info@malindians.com indicating the proposed changes and the content URL(link). Provide as much information as you can and we promise to take corrective measures to the best of our abilities.

Komzinski is a Research and Monitoring Assistant at the Northern Rangelands Trust (NRT). He enjoys the outdoors and travelling. When not travelling, Athuman enjoys volunteering at the local beach management unit, playing soccer, and coding together with friends planning on their next tech startup project.

Comments

Trending

Bloggers Association of Kenya Tracker
%d bloggers like this: