Katoi Wa Tabaka – Malindi Music

Katoi wa Tabaka ni jina  linaongelea kimo na miaka lakini sio mtazamo wenyewe ikilinganishwa na kichwa alichokibeba msanii huyu chenye uwezo mkubwa wa ubunifu na ujanja wa hali ya juu.

Katoi wa Tabaka anajulikana rasmi kama Katoi Mathiaspato na amekuwa kwenye kikundi cha TABAKA akiwa na Mbuyu. Kama Kikundi cha Tabaka, wamekuwa waanzilishi wa mziki wa hip hop mkoani pwani kwa jumla.

Kama msanii na mkereketwa mkuu wa tamaduni ya kigiriama, Katoi wa Tabaka amekuwa akipigania vikali kudumishwa kwa mila na tamaduni za mijikenda mjini Malindi na kwengine kupitia mtindo wake mwenyewe wa hiphop anaouita “Kaya Hiphop”.

Msanii huyu kwa sasa ameachilia album yake itwayo KAYA MUSIC na kutayarisha nyimbo ziliziko kwa album hiyo kupitia studio tofauti ughaibuni.Msanii huyu amewahi kuwa mkaazi wa Roma, Italy na amewahi fanya collabo kadha na wasanii wa Italy kama vile Giulia ugatti acoustic soul singer na Enose Dee mkenya anaeishi Rome.

{
“@context”: “http://schema.org/”,
“@type”: “Person”,
“name”: “Katoi Mathiaspato”,
“alternateName”: “Katoi wa Tabaka”,
“url”: “https://malindians.com/people/cfree-chrisborn/”,
“image”: “http://blog.malindians.com/wp-content/uploads/2018/11/cfree-chrisborn.jpg”,
“jobTitle”: “Artist”
}

We will be happy to hear your thoughts

Share your thoughts in the comment below.

Bloggers Association of Kenya Tracker