Tambi za Nazi ni moja wapo wa mapishi ya tambi ambao tambi hupikwa kwa kuchanganya tui la nazi. Upishi huu ni maarufu sehemu kadhaa pwani ya kenya
Tambi ni neno linalojumuisha aina nyingi ya mapishi ya watu wa pwani ya kenya na kwa jumla Africa Mashariki yote. Tambi ni hutengenezwa haswa haswa na ngano iliyokandwa na kufanya kama kambaa nyembamba. Hizi kambaa nyemba hukaushwa na kuachwa tayari kupika. Aina ya tambi hulingana na aina ya mapishi ya tambi. Tambi zinazopikwa na nazi huitwa Tambi za nazi, tambi zilizopikwa pamoja na nyama ya kusagwa huitwa tambi za nyama ya kusagwa na kadhalika.
Vile vile kambaa nyembamba za tambi hutengeneza na mali ghafi tofauti na ngano. Tambi zinaweza kutengenezwa na papai, mchele au hata dengu.
VIPIMO
- Tambi za Mchele
- Pakti 1 (400 mg)
- Tui la nazi Kikombe 1
- Sukari Nusu kikombe, ukipenda ongeza kidogo
- Maziwa ya kopo (evaporated) Nusu kikombe
- Samli Kijiko 1 cha supu
- Zabibu kavu ¼ Kikombe
- liki
- ¼ kijiko cha chai ‘Arki (rose flavour) Matone matatu au zaidi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Chemsha tambi kidogo tu katika maji yanayochemka na uzichuje (zisiwive)
- Chemsha tui la nazi, pamoja na vitu vyote vingine, koroga vichanganyike katika moto.
- Tia tambi na koroga vizuri.
- Karibu na kukauka tui mimina tambi katika treya ya kupikia na zitie katika jiko (oven) zipike kwa moto wa 350 Deg. mpaka zikauke. (kama dakika 15 ) Kisha zima moto wa chini na washa moto wa juu zigeuge rangi kidogo.
- Ziepue na zipakue katika sahani zikiwa tayari kuliwa.