Tambi za Kukaanga – Recipe za Ramadhan
Mapishi

Tambi za Kukaanga – Recipe za Ramadhan

komzinski
komzinski Travel Writer & Local Guide
Jul 16, 2020 5 min read 29 views

Vipimo vya Tambi za Kukaanga

Tambi pakti moja

Sukari ¾ kikombe cha chai

Mafuta ½ kikombe cha chai

Iliki kiasi

Maji 3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose 1-2 Tone

Zabibu Kiasi (Ukipenda)

Namna ya kutayarisha na kupika Tambi za Kukaanga

Zichambue tambi ziwe moja moja.

Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto.

Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.

Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

 

 

Kidokezi kuhusu Tambi za Kukaanga

Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.


Discover more from Malindians

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Enjoyed this article?

Subscribe to get more stories like this delivered to your inbox every week.