Connect with us

Mapishi

Juice ya embe – Recipe za Malindi

Published

on

Juice ya embe - Recipe za Malindi

Maembe au tunda la embe in mojawapo wa matunda ambayo yanafahamika na kupendwa na idadi kubwa ya watu. Watu wengi hula tunda hili la embe moja kwa moja au kutengeneza juice.

  • Maembe yaliyoiva 2
  • Mtindi (yoghurt) 2 Vikombe vya chai
  • Maziwa 1 Kikombe cha chai
  • Asali au Sukari ¼ Kikombe cha chai
  • Maji ya ndimu ½ Kipande
  • Barafu 12 vipande
  • Mdalasini ya unga kidogo

Namna ya kutayarisha Juice ya embe

Menya maembe yako kisha ukate kate vipande.

Weka vipimo vyote vilivyopo hapo juu isipokuwa mdalasini, kwenye mashine ya kusagia (blender).

Saga hadi ilainike.

Mimina kwenye gilasi na unyunyize mdalasini kidogobaada ya hatua hizo juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa

READ  Juice ya Embe na Passion – Recipes za watu wa Malindi

Komzinski ni mfanyakazi katika shirika lisilo la kiserikali la Northern Rangelands Trust (NRT). Anapenda mazingira na kujifunza kuhusu tamaduni mbali mbali kupitia safari na pilkapilka zake nyingi

Continue Reading
Comments

Trending

Copyright © 2020 All Rights Reserved | Malindians.com

Bloggers Association of Kenya Tracker