Maembe au tunda la embe in mojawapo wa matunda ambayo yanafahamika na kupendwa na idadi kubwa ya watu. Watu wengi hula tunda hili la embe moja kwa moja au kutengeneza juice.
- Maembe yaliyoiva 2
- Mtindi (yoghurt) 2 Vikombe vya chai
- Maziwa 1 Kikombe cha chai
- Asali au Sukari ¼ Kikombe cha chai
- Maji ya ndimu ½ Kipande
- Barafu 12 vipande
- Mdalasini ya unga kidogo
Namna ya kutayarisha Juice ya embe
Menya maembe yako kisha ukate kate vipande.
Weka vipimo vyote vilivyopo hapo juu isipokuwa mdalasini, kwenye mashine ya kusagia (blender).
Saga hadi ilainike.
Mimina kwenye gilasi na unyunyize mdalasini kidogobaada ya hatua hizo juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.