Mji wa Malindi unatambulika hapo zamani kama Melinde. Mji huu upo katika Kaunti ya Kilifi (Kaunti 003) katika Jamhuri ya Kenya. Kwa muujibu wa mwana jeografia wa asili ya Kikurdi, Abu Al-Fida(1273-1331), Malindi mji ambao uko kusini wa mto Sabaki ulianzishwa kati ya karne ya 13-14.
Chanzo cha kuimarishwa kwa mji wa Malindi ni kuja wa wafanyi biashara wa asili ya kiarabu ambao baada ya kukazaa na wenyeji ndio ikaleta chimbuko la kabila ya Waswahili mwisho wa karne ya 13.