Mr. Boniface ni tamthilia fupi iliyotengenezwa mjini Malindi. Inazungukia maisha ya mwalimu Boniface aka Mr.Boniface, ambaye ni mwalimu wa somo la hesabati katika shule ya msingi ya Bonde Ziwi.
Shule ya Msingi ya Bonde Ziwi inanikumbusha jinsi shule za msingi zilivyokuwa miaka ya 90, wakati walimu walitumia viboko kuwatia nidhamu wanafunzi waliokuwa na vichwa vigumu.
Mr. Boniface Season 1 Episode 1
Katika episode hii ya kwanza, Mr. Boniface anatambulishwa kama Mwalimu wa hesabu asiyependa mchezo hata kidogo. Darasa lake la sita liko na wanafunzi wa aina tofauti; waliokuwa na bidii darasani na wale ambao wako na shida tele majumbani ambazo zimewafanya kukosa makini wakiwa darasani. Mr Boniface, hachelei kutumia kiboko kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi amenyooka.