Tambi za Nazi – Recipe za watu wa Malindi

TAMBI ZA NAZI

VIPIMO

 1. Tambi za Mchele
 2. Pakti 1 (400 mg)
 3. Tui la nazi Kikombe 1
 4. Sukari Nusu kikombe, ukipenda ongeza kidogo
 5. Maziwa ya kopo (evaporated) Nusu kikombe
 6. Samli Kijiko 1 cha supu
 7. Zabibu kavu ¼ Kikombe
 8. liki
 9. ¼ kijiko cha chai ‘Arki (rose flavour) Matone matatu au zaidi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 1. Chemsha tambi kidogo tu katika maji yanayochemka na uzichuje (zisiwive)
 2. Chemsha tui la nazi, pamoja na vitu vyote vingine, koroga vichanganyike katika moto.
 3. Tia tambi na koroga vizuri.
 4. Karibu na kukauka tui mimina tambi katika treya ya kupikia na zitie katika jiko (oven) zipike kwa moto wa 350 Deg. mpaka zikauke. (kama dakika 15 ) Kisha zima moto wa chini na washa moto wa juu zigeuge rangi kidogo.
 5. Ziepue na zipakue katika sahani zikiwa tayari kuliwa.

We endeavor to keep our content True, Accurate, Correct, Original and Up to Date.If you believe that any information in this article is Incorrect, Incomplete, Plagiarised, violates your Copyright right or you want to propose an update, please send us an email to info@malindians.com indicating the proposed changes and the content URL(link). Provide as much information as you can and we promise to take corrective measures to the best of our abilities.

Share your thoughts in the comment below.

Bloggers Association of Kenya Tracker
%d bloggers like this: