Ghazah Street Don – Kutumia mziki kuhamasisha Jamii

Ghazah Street Don , ni mwanamuziki anaye fanya hiphop na Rnb mjini Malindi Kenya huku akijivunia kuja na mtindo wake spesheli wa reggae RnB. Faris Saraya Kombe, kama anavyojulikana rasmi ni mzaliwa na mkazi wa mji wa Malindi, mitaa ya Muyeye.

Amekuwa akifanya kazi na studio kadhaa kama vile Street Beat akiishirikisha Inspyce Records na vile vile akiwa na kikundi cha Krayzano legend. Krayzano Legend anavyodai ni kikundi ambacho amekuwa akikishikilia mkono ili kupata kuinua talanta.

Alianza mziki kwa kuandika rhymes na mashairi kadhaa kuanzia alipokuwa shule miaka ya nyuma. Baada ya kujulia zaidi alisema ilikuwa mwaka wa 2005 ambapo aligundua ako na kipaji ya utunzi. Baada ya miaka kadhaa ya utunzi, aliamua kuingia ndani ya studio na kuanza kurekodi.

Mapenzi ya Mziki

Mziki kwake unahamasisha na funza jamii na pia kuumpa ari ya kuendelea na kuchapa kazi kimaisha. Kitu kikubwa kilichochangia wewe kuingia ndani ya ulingo wa sanaa ilikuwa ni kufuata nyayo za kakake mkubwa anayejulikana kama Mitaa Kisauni. Kuingia kwake ndani ya sanaa ya mziki pia kulifanya mdogo wake, Green Boy, kuingia ndani ya mziki pia.

Kazi zake

Kuanzia mwaka wa 2011, ameweza kutoa nyimbo zisizopungua kumi na tano (15) na album moja – Siri yangu. Safari ya mziki wake imekuwa na changamoto kadhaa, na hii imechangia wewe kujifunza ufundi wa kutengeneza nyimbo (producer), ufundi ambao ameanza kuujenga ndani ya Studio ya Malindi Records. Akiwa Malindi Records alipatana Producer Sango ambaye alimtambulisha kwa Universal Studio ambayo ilikuwa Black Legend na hatimaye kumaliza kazi zake nyingi Inspyce Records.

We endeavor to keep our content True, Accurate, Correct, Original and Up to Date.If you believe that any information in this article is Incorrect, Incomplete, Plagiarised, violates your Copyright right or you want to propose an update, please send us an email to info@malindians.com indicating the proposed changes and the content URL(link). Provide as much information as you can and we promise to take corrective measures to the best of our abilities.

Share your thoughts in the comment below.

Bloggers Association of Kenya Tracker