Bloggers Association of Kenya Tracker
Connect with us

Mapishi

Visheti – Recipe za Eid

Published

on

mapishi ya visheti

Wadau wa jiko letu, leo tuna visheti. Visheti ni aina ya kitafunwa, chaweza liwa na kahawa, chai, juisi na hata maji . Ila kwa chai na kahawa vinapendeza zaidi. Kuna namna tofauti tofauti za uandaaji wa visheti, kukandia nazi, mara nyengine mafuta, waweza pia kukandia siagi na hata maziwa. Vya leo tutatumia siagi, na tukijaaliwa siku nyengine tutapika na hizo aina nyengine.

visheti malindians.com  - Visheti - Recipe za Eid

Mahitaji ya Kuandaa Visheti

Ngano kilo1

mafuta lita1

siagi robo kilo

yai 1

Hiliki kiasi

baking powder kijiko1

Chumvi kidogo sana

Sukari nusu

JINSI YA KUPIKA Visheti

Chunga unga wako, weka baking powder, tia chumvi kidogo ukipenda, tia sukari kidogo na hiliki changanya na siagi uvurugetia mafuta nusu kikombe, endelea kuvuruga unga wakopiga yai litie kwenye unga, endelea kuvurugaongeza maji kiasi ili unga wetu uweze kukandika na kushikana kuwa donge moja.

Tengeneza vidonge vidonge, kisha uviviringishe hadi viwe kama fimbo, baadae weka kwenye kibao ukatekate visheti vidogo dogo

Weka mafuta kwenye karai jikoni, yakipata moto kaanga visheti hadi viive, kisha vitoe pembeni uanze kuandaa SHIRA

Andaa shira kwa kutumia sukari nusu, na maji kikombe cha chupa ya chai kimoja, bandika jikoni maji ulotia sukari yachemke hadi yatoe povu na ukiitoa kidogo ukiishika inanata sana, hapo shira ni tayarimimina visheti ulokaanga kwenye sufuria ya shira, weka na hiliki, kisha vipetepete ili vijigeuze na kuenea sukari vyote. Vikiwa tayari vimekaukia sukari vizuri, visheti vyetu weka kwenye chombo tayari kumfikia mlaji

Visheti vyetu tayari wadau, mimi huvipenda hivi vya kukandia siagi sababu hukaa muda mrefu bila kuwa vigumu. Kwa hiyo waweza tengeneza ukala na vikibaki unavihifadhi vizuri kwa ajili ya kutafuna siku nyengine.

Komzinski ni mfanyakazi katika shirika lisilo la kiserikali la Northern Rangelands Trust (NRT). Anapenda mazingira na kujifunza kuhusu tamaduni mbali mbali kupitia safari na pilkapilka zake nyingi

Comments

Facebook

Proud Member

Bloggers Association of Kenya Badge
Advertisement

Trending

Bloggers Association of Kenya Tracker
%d bloggers like this: