Mapishi
Tambi za Kukaanga – Recipe za Ramadhan

Vipimo vya Tambi za Kukaanga
Tambi pakti moja
Sukari ¾ kikombe cha chai
Mafuta ½ kikombe cha chai
Iliki kiasi
Maji 3 Vikombe vya chai
Vanilla / Arki rose 1-2 Tone
Zabibu Kiasi (Ukipenda)
Namna ya kutayarisha na kupika Tambi za Kukaanga
Zichambue tambi ziwe moja moja.
Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.
Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.
Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto.
Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.
Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa
Kidokezi kuhusu Tambi za Kukaanga
Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.
-
Mapishi3 miaka ago
Biriani ya mbuzi – Recipes za watu wa Malindi
-
Mapishi1 mwaka ago
Juice ya Embe na Passion – Recipes za watu wa Malindi
-
Mapishi1 mwaka ago
Bhajia za Kunde
-
2 miaka ago
Ghazah Street Don – Kutumia mziki kuhamasisha Jamii
-
Mapishimiezi 12 ago
Mikate Ya Maji Ilojazwa Nutella – Malindi Recipes
-
Mapishimiezi 9 ago
Juisi ya nanasi na tango
-
Videosmiezi 11 ago
Tamthilia ya Mr. Boniface – Season 1 Episode 2
-
Burudanimiezi 9 ago
Tamthilia ya Mr. Boniface – Season 1 Episode 4