Mikate Ya Maji Ilojazwa Nutella – Malindi Recipes

Mikate ya maji iliyojazwa nutella (crepes), ni miepesi kuliko kawaida. Nutella inatandaza kwa mkate hii na kuipatia ladha murua kabisa. Aina hii ya vyakula huliwa wakati wowote ule.

Nutella ni nini?

Nutella ni mchanganyiko wa chocolate na Hazel(hazelnut). Jinsi inavyotengeneza katika viwanda haiko tofauti sana na vile inavyotengenezwa majumbani.

Nutella inatengenezwa kutumia sukari, mafuta ya nazi, hazel, unga wa cocoa, maziwa ya unga, soya, vanila, lecithin and unga wa whey.

Kwanini watu wanapenda mikate ya Maji

Mikate ya maji(crepes) ya aina hii inawezwa kupaka chochote kile, chachu au tamu. Kulingana na upishi, inaweza kuwa miepesi kuliko mikate ya maji mingine, mitamu na yenye kushibisha.

VIPIMO:

⚫Unga wa cake kikombe 1⅓
⚫Maziwa kikombe 1
⚫Maji ½ kikombe
⚫Sukari ¼ kikombe
⚫Yai 1
⚫Chumvi 1/4 kijiko chai
⚫Mafuta ya kula kwa ajili ya kupakaza chuma
⚫Nutella kwa ajili ya kujaza
⚫Chocolate ya nutella iloyeyushwa (ukipenda)

MAELEKEZO:-

1. Katika bakuli ya kati tia Mahitaji yote kisha piga hadi mchanganyiko uwe smooth.

2. Tia chuma chako ulichokipaka mafuta jikoni katika moto wa kiasi.

4. Minina unga wako wa mikate ya maji ktk chuma chako,chota 1/4 kikombe ya unga kwa kila mkate.

5. Zungusha chuma chako kueneza unga wako na kufanya duara.

6. Pika mkate wako kwa sekunde 30 au hadi chini ipate rangi.

7. Geuza upande wa pili kwa kutumia spatula kisha acha na upande wa pili upate kuiva,epua ktk sahani, Rudia kumaliza unga wote.

8. Paka Nutella juu ya mkate wako isiwe nyingi sana kisha zungusha kama picha inavyoonyesha. Utarudia kwa zote

9. Pambia kwa kunyunyiza chocolate uloyeyusha (ukipenda)

Note:
Unga wa crepe au mikate ya Maji hasa unayojaza inatakiwa uwe mwepesi zaidi

Fungua comments uone namna ya kukunja na hiyo nutella kwa wasioijua

Rejea post za nyuma kuona namna gani unaweza kutengeneza unga wa cake nyumbani

{{CODECreppesSchema}}

We endeavor to keep our content True, Accurate, Correct, Original and Up to Date.If you believe that any information in this article is Incorrect, Incomplete, Plagiarised, violates your Copyright right or you want to propose an update, please send us an email to info@malindians.com indicating the proposed changes and the content URL(link). Provide as much information as you can and we promise to take corrective measures to the best of our abilities.

Share your thoughts in the comment below.

Bloggers Association of Kenya Tracker