Mapishi
Katlesi za Samaki – Recipe za Ramadhan

Vipimo vya kuandaa Katlesi za Samaki
Viazi – 5 kiasi
Tuna – 2 vikopo
Carrot – 1
Pilipili mboga – Nusu
Kitunguu saumu(thomu/garlic) – ½ kijiko cha chai
Pilipili – kiasi
Chumvi – kiasi
Ndimu – kiasi
Unga wa ngano – ½ kikombe
Yai – 1
Mafuta ya kupikia – Kiasi
Namna ya kutayarisha na kupika Katlesi za Samaki
Menya Viazi uvichemshe na chumvi.
Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie – weka kando
Chuna carrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga nyembamba nyembamba, fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga.Changanya Tuna, carrot, pilipili mb
oga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu, kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika vizuri.
Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.
Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.
Weka karai katika moto, mimina mafuta kama ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.
Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula.
-
Mapishi3 miaka ago
Biriani ya mbuzi – Recipes za watu wa Malindi
-
Mapishimiezi 12 ago
Juice ya Embe na Passion – Recipes za watu wa Malindi
-
Mapishimiezi 12 ago
Bhajia za Kunde
-
2 miaka ago
Ghazah Street Don – Kutumia mziki kuhamasisha Jamii
-
Mapishimiezi 12 ago
Mikate Ya Maji Ilojazwa Nutella – Malindi Recipes
-
Mapishimiezi 9 ago
Juisi ya nanasi na tango
-
Videosmiezi 11 ago
Tamthilia ya Mr. Boniface – Season 1 Episode 2
-
Burudanimiezi 9 ago
Tamthilia ya Mr. Boniface – Season 1 Episode 4