Home Recipes Watermelon Juice

Watermelon Juice

by komzinski
juice ya watermelon - malindians

Perfect drink for your summer, waandalie familia wafurahie pia kama unabiashara waandalie wateja wako wafurahie sana hasa kipindi hiki cha majira ya joto.

Jinsi ya kutengeneza Watermelon juice (juisi ya tikiti maji)

Mahitaji

  • 450 grams Vipande vya Watermelon vyenye ubaridi,
  • 250 gram ya maji ya dafu au Nazi changa
  • 1 limao kubwa
  • 10 vipande vya barafu au Ice cubes,
  • Fresh Mint kwajili ya kupambia

 

Jinsi ya kutengeneza watermelon juice (juisi ya tikiti maji) na limao

  1. Kata nusu tikiti maji zuri lililoiva kama unavyoona kwenye picha kisha likate kate vipande na uweke kwenye friji vipoe kabla ya kutengeneza juisi yako
  2. Chukua maji ya dafu, limao, vipande vya barafu na vipande vya tikiti maji kisha weka kwenye blender.
  3. Lengo la kuweka limao ni kuongeza na kubalance ladha. kama wewe ni mpenzi sana wa maji ya madafu unaweza ongeza zaidi ili ladha ya madafu isikike sana.
  4. Blend vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike safi kabisa. Perfect drink for your summer, waandalie familia wafurahie pia kama unabiashara waandalie wateja wako wafurahie sana hasa kipindi hiki cha majira ya joto. kumbuka tikiti maji na dafu vyote vinasukari kwahiyo huna haja ya kuongeza sukari kabisa na ukafurahia kinywaji hiki murua.


Discover more from Malindians.com

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More