Juice ya Embe na Passion – Recipes za watu wa Malindi

0
1646
recipes-ya-juice-ya-embe-na-passion - malindians

Joto na vuke kama wanavyosema wakaazi wa malindi ni kawaida ya “Malindi weather”. Wengi hupenda kujiburudisha na kinywaji baridi ili kupunguza makali ya jua. Juice na embe, passion au sharubati zingine ni maarufu sana sehemu hizi za pwani. Leo nimeamua kuwaandalia juice mchanganyiko wa juice ya embe na passion.

Mango and passion juice recipe - Juice ya Embe na Passion – Recipes za watu wa Malindi

Jinsi ya  kutengeneza juice ya embe na passion

Vipimo:

Passion fruit  8

Embe  6 za kiasi

Maji  kiasi

Sukari  kiasi upendavyo

Namna Ya Kutayarisha

1.  Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje .

2.  Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.

3.  Tia sukari korogo  ikiwa tayari.

See also:   Bhajia za Kunde