Easy buns – Recipes za Watu wa Malindi

0
858
easy buns on malindians.com

VIPIMO:

Unga wa ngano vikombe 3 1/4
Sukari vijiko 2 chakula
Chumvi kijiko 1 chai
Hamira vijiko 3 chai
Maziwa ya unga vijiko 2 chakula (ukipenda)
Maji vugu vugu kikombe 1 1/4
Siagi vijiko 2 chakula

NAMNA YA KUPIKA

1. Tia mahitaji yote katika bakuli isipokuwa siagi kisha kanda kwa dakika 5.

2. Tia siagi kisha kanda unga wako kwa dakika 10 hadi uwe mlaini na wakuvutika.

3. Tia katika bakuli ulopaka mafuta au siagi, funikia na plastic au kitambaa acha ufure kwa muda wa dakika 30.

4. Kanda kwa dakika 1 kisha gawa vipande na kisha fanya maduara. Panga katika tray ulopaka mafuta.

5. Funikia tena acha zifure kwa dakika 30. Oka katika oven ya moto joto 180°c kwa muda wa dakika 20 au hadi zipate rangi ya brown juu.

6. Paka siagi juu zikiwa bado moto. Enjoy!

Note:
Weza paka egg wash juu ya buns kabla ya kuoka (piga yai 1+ kijiko 1 Maji)

 

Leave a Reply