Producer Sango

Anajulikana kama Ramadhan Athman Salim, majina ambayo yamwo katika kitambulisho cha taifa. Lakini katika ulingo wa sanaa anatambulika kama Sango. Sango ni mzaliwa na mkazi wa mji wa Malindi. Jina la Sango anavyosema yeye limetokana na wimbo uliopenda sana na bibi (nyanya) yake.

Sango ni producer wa mziki; kazi ambayo amekuwa akiifanya kutoka 2013. Alianza kazi hii baada ya kupendezwa na kazi ya usanii wa kuimba alipokuwa shule ya Upili ya Pwani, mitaa ya Kosovo barabara ya Tsavo. Japo hakuwahi ingia studio kurekodi, alikuwa akiandikia mashairi wasanii wenzake katika Studio ya Black Legend, hapo kwa Fundi Konde mitaa ya Kisumu Ndogo

Producer Sango - Sanaa za Malindi
Producer Sango Akiongelea kuhusu Changamoto zinazokumba ulingo wa sanaa ya Kuimba

Safari yake ya mziki kama Producer

Baada ya Kutoka black Legend amewahi kufanya kazi na studio ya Malindi Records Record and Inspyce Records.

Ndoto ya Mziki

Producer Sango alianza kupenda mziki Kipindi alipokuwa akisoma Madrassa mjini Matsangoni. Kipindi hichi alipenda sana Qaswida, kupiga matwari na kasba.

Changamoto

Changamoto za mziki zipo nyingi. Anasema safari ya kuwa Producer si rahisi kwani mtu hukesha kwa masaa mengi akijaribu kupata ujuzi unaostahili.

“Mimi nimeng’atwa na mbu nikifanyia Wasanii Mastering ya kazi zao” – Producer Sango

Anasema changamoto zingine anazopambana nazo zipo kwenye wasanii wenyewe. Wengi wanaohuchukua muda mrefu kuingiliana na kanuni za mziki na wanakosa subira ya kutekeleza mambo kadhaa.

Ruwaza na Malengo kuhusu sanaa ya mziki Malindi

Anatazamia kufungua shule ya kufundisha mziki. Katika shule hii atakuwa akisaidia kuinua vipaji vya wanamziki na pia vile vile ma produder wengine.

Kazi za Producer Sango

Sango ameweza kufanya pamoja na wasanii wengi na “kupika” kazi chungu mzima ndani na nje ya Malindi Baadhi yao ni:-

  1. SwankyMurder Me
  2. Young Njita
  3. Mbekas
  4. Passion AYK
  5. Bozen AYK
We endeavor to keep our content True, Accurate, Correct, Original and Up to Date.If you believe that any information in this article is Incorrect, Incomplete, Plagiarised, violates your Copyright right or you want to propose an update, please send us an email to info@malindians.com indicating the proposed changes and the content URL(link). Provide as much information as you can and we promise to take corrective measures to the best of our abilities.

1 thought on “Producer Sango”

Share your thoughts in the comment below.

Bloggers Association of Kenya Tracker