Jina la kwangu kwa mziki ni Mc Newton mzaliwa wa Malindi. Newton sio jina nilopewa wa wazazi kwa jina lao waniita Lewis ambapo kwa bidii ki mziki watu wakifika nyumbani huulizia Newton basi ikawa lazimu paka leo huniita Newton.
Mziki wangu ni U.G.H (Underground) hiphop unaoelezea hisia tofauti za maisha ya kila siku na kusimamia haki.
Umefanya Sanaa kwa muda gani?
Revolution nilianza kitambo, kipindi kisichopungua miaka 6, ambacho nimekuwa nikifanya studio recordings.
Unajivunia nini Kwa kipindi hichi?
Zipo faida nyinyi ninazopata na zinazoendana na U.G.H japo kati ya yote ninapoona watu wanatamani kazi mpya na wanaheshimu kazi zangu mtaani ya Badlands more love iko naamini hii ndo njia pekee yakufikia pesa. With respect comes the cash.
Changamoto ya mziki
Mziki changamoto zake ni hela tu. Ukiwa na kipaji na hauna hela uongo labda kwa huruma na bahati kutoka kwa Mwenyezi. Ila kwa maisha yenyewe ukisikia mziki ni biashara jua biashara lazima mtaji(capital).
Mawaidha
So nikipata nafasi ya kuwambia wanaotamani kuingia kwa game, Kama wapo shule wasome wamalize kwani kipaji hakizeeki, na walio kwa mziki mtafute kazi tofauti tusukume maisha, pia ma producer ni wazazi wana watoto wanataka kuja na kusoma. So tafuta hela mziki si mgumu ila ukikataa kusikiza wao kuwa mwanzoni utafikia mahali uchanganyikiwe..
Nawapenda sawa team SHANDELA
Contacts Zako?
Unaeza ni follow Instagram mc_Newton 254 na Facebook mc Newton
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.