Home People of Malindi David Mafishy – Mtangazaji na msanii wa vichekesho

David Mafishy – Mtangazaji na msanii wa vichekesho

by komzinski
mafishy masamaki aka Mr. Boniface

David Mafishy Masamaki ni mmoja wapo wa wasanii wanaofanya tasnia ya vichekesho mjini Malindi. Mzaliwa wa Kaunti ya Kiifi, mji wa Malindi katika mtaa wa Ngala, David Mafishy anajulikana rasmi kama David Ng’anga Njenga. David Mafishy anavijunia kutoka katika jamii ya mijikenda licha ya kuwa na majina ya N’gang’a na Njenga ambayo chimbuko lao si pwani mwa Kenya, bali mkoa wa Kati. Hii inatokona na kulelewa na familia ya mama pekee na asiweze kumjua babake mzazi kutoka kuzaliwa kwake.

Elimu ya David Mafishy

David Mafishy alianza masomo yake masomo ya msingi katika shule ya Upweoni, mtaa wa Ngala na hatimaye kumaliza katika shule ya HGM mwaka wa 2005 ilioyoko mtaa wa Kisumu Ndogo. Alijiunga na Shule ya Upili ya Gede Secondary School mwaka wa 2006 na hatimaye kumaliza mwaka 2010 katika shule ya Brilliance.

Kuanza kwa sanaa kwa David Mafishy

Shule ya upili ya Brilliance ilikuwa na drama club ambayo aliunga nayo mwaka wa 2009 alipokuwa kidato cha tatu. Drama club ilikuwa ikiongozwa na jamii ya kiislamu katika shule hiyo kwa sababu ya mashindani waliyokuwa nayo. Lakini hili halikumrudisha nyuma au wala kuwa pingamizi yoyote kwa Mafishi kujitosa katika sanaa.

Baada ya kumaliza shule ya Upili, alijiunga na waigizaji wengine kama vile Sule Mpenz na kuanzisha Tujumuike Sanaa group. Baada ya mwaka, walijiunga na Mango Mango msanii mcheshi muigizaji. Baada ya mwaka mmoja kikundi hicho kilianza kutengeza filamu fupi za vichekesho baada ya kuungana na Medu Dume wa Malindi Movie Majic.

Tamasha la Hiphop Beyond the Mic lilimpatia  David Mafishi fursa ya kufanya stand-up comedy kwa mara ya kwanza maishani mwake na hio ndio ikawa ufunguo kwa mambo mengi yaliofuatia baadae.

Faida ya Sanaa Kwa David Mafishy

Sanaa ya comedy imemlea David mafishi and imekuwa na faida nyingi sana maishani. Kwake binafsi ametaja mifano kadhaa ambayo imedhibitisha sanaa inaweza kutengemewa na kuendeza maisha ya msanii.

Changamoto

Changamoto kubwa kwake ni kuwa mbunifu kuja na vichekesho tofauti tofauti. Zamani alipoanza comedy alikuwa akifanya aina nyingi ya comedy,ila tu alipobadilisha na kuanza kufanya comedy kwa lugha ya kigiriama, mambo yamekuwa nafuu.
Changamoto ya pili ni uhaba wa pesa kufanikisha sanaa yake, kwani kupata kusikika vizuri inahitaji kutengeneza video kadhaa ambazo ziko na gharama.
Wasanii wenza wamekuwa changamoto pia kwenye industry. Roho chafu za wasanii wenza amesema pia kuwa ni moja wapo wa changamoto zinazomkumba yeye. Anahisi wasanii wamekuwa wakichangia kuanguka kwa wasanii wenzao.

Mawaidha

Hakuna kitu kinachofanyika kwa siku moja. Lazima mtu awe mvumilivu sana kwani kuwa kunatoka semi nyingi ambazo zinavunja moyo. Kama msanii unafaa kutumia semi hizi za kuvungu moyo na kuzibadilisha ziwe za kukupeleka mbele.

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More