PEOPLE OF MALINDI
Bryba – Msanii kutoka Watamu

Bryba ni msanii wa kuimba kutoka mji wa Watamu katika kaunti ya Kilifi.
Safari ya msanii Bryba katika ulingo wa sanaa ya kuimba ilianza tu baada ya kumaliza masomo ya shule ya upili mwaka wa 2013. Tangu hapo ameweza kufanya kazi kadhaa ikiwemo video moja.
Mapenzi ya mziki
Bryba anadai chimbuko lake la mziki lilianza akiwa shuleni. Marafiki wake wa shule na machizi mtaani ndio waliokuwa sababu kubwa yake kuingia ndani ya sanaa ya mziki. Hii ilimfanya kuanza kuimba shuleni na wakati wowote anapata akiwa mtaani.
Mentor wa Bryba katika muziki
Bryba ametilia mkazo sana nafasi iliyochezwa na Sudi boy katika maisha yake na vile vile safari yake ya mziki. Anadai kuwa Sudi Boy amekuwa “Role model” wake na pia mentor ni Sudi Boy huku akicheza nafasi kubwa katika safari iliyomfikisha pale alipo sasa.
Mchango wa Sanaa katika Maisha
Sanaa imemfika alipo sasa na anasema kika siku anazidi kukua kama msanii ila changamoto zipo kibao. Changamoto kubwa ni kipato kidogo cha hela. Anakiri kuwa kila kitu kinazukia pesa na bila huwezi fanya kitu. Hili halijamfanya Bryba apunguze bidii katika kazi ilo ili awaze kufanisha malengo
Matarajio kwa Mashabiki?
Anataka mashabiki wake watarajie video kadhaa mwaka huu. Vile vile anaahidi collabo chungu mzima (amebana majina ya kazi hizo na wale ambao atawashirikisha). Lakini kazi hizi zitamfanya apande katika anga ya mziki.
-
Lifestyle2 years ago
7 outfit ideas for men on Malindi Beaches
-
Events1 year ago
My take of 2nd Edition of the Malindi Business & Art Exhibition
-
Travel guides2 years ago
No bra day – the best reason to take it off
-
Travel guides1 year ago
7 Best hotels in Malindi to check out in 2020
-
PEOPLE OF MALINDI7 years ago
Iman Sidi Katanu
-
PEOPLE OF MALINDI2 years ago
Haifa AbdulHakim Awadh Timimi
-
Travel guides2 years ago
The Unsolved Mystery of Gedi Ruins
-
PEOPLE OF MALINDI3 years ago
Asfat AbdulRazaq