Home Mapishi Maandazi ya Nazi

Maandazi ya Nazi

by komzinski
maandazi-recipes-malindians

Tukiwa katika “countdown” ya siku hadi Mwezi mtukufu wa Ramadhan, matayarisho kabambe tayari yashaanza kufanywa hasa pande zetu za uswahilini. Mapishi huwa ni sehemu muhimu katika jamii zetu. Huku pwani, mapishi ni kivutio kikubwa. Malindians tukishirikiana na Mapishi mix tutakuwa tukiwaletea resipe (Recipes) ya vyakula tofauti tofauti.

Vipimo
Maji ½ kikombe

Hamira vijiko 2 1/4 chai

Tui la nazi zito kikombe 1

Ute wa mayai 2

Sukari ½ kikimbe

Chumvi kijiko 1 chai

Unga wa ngano vikombe 3½ – 4

Nazi iliyokunwa ¼ kikombe

Hiliki iliyotwangwa kijiko 1 chai

Kungu manga ilokunwa kijiko 1 chai

Sukari ya unga kwa ajili ya kunyunyiza juu(ukipenda)

Mafuta ya kukaangia

 

maandazi-recipes-malindians

MAELEKEZO:
1. Tia Maji katika sufuria jikoni acha yapate moto, kisha mimina katika bakuli kubwa yakiwa moto, tia tui la nazi, chumv na sukari koroga vizuri kisha tia hamira koroga tena acha ifure kwa muda wa dk 5.

2. Tia ute wa mayai koroga vizuri , kisha tia vikombe 3 1/2 unga, hiriki,kungu manga na nazi ya kukuna kisha endelea kuchanganya kwa mkono au mashine hadi ufanye donge.

3. Kanda unga wako hadi uwe laini na wakuvutika, ongeza unga kidogo kama utakuwa wakunata hakikisha hauzidishi unga ukawa mkavu sana.

4. Tia unga wako katika bakuli ulopaka mafuta ,funikia kwa plastic au kitambaa kisafi kisha acha ufure hadi ujae mara mbili.

5. Sukuma unga wako kufanya chapati pembe nne yanye unene kama inch 1 kisha kata maandazi yako kama picha inavyoonyesha ,unaweza pia kata kwa style yoyote upendayo.

6. Mimina mafuta katika sufuria yako, tia jikoni katika moto wa kiasi yapate moto.

7. Kaanga maandazi yako hadi yapate rangi ya brown pande zote mbili. Epua acha yachuje mafuta katika paper towel au wire rack. Rudia kumaliza yote.

8. Nyunyiza sukari ya unga ukipenda, Kula maandazi yako kwa kikombe cha kahawa pembeni. Enjoy!

For our English readers, here is the recipe:

 

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More

Privacy & Cookies Policy