Joto na vuke kama wanavyosema wakaazi wa malindi ni kawaida ya “Malindi weather”. Wengi hupenda kujiburudisha na kinywaji baridi ili kupunguza makali ya jua. Juice na embe, passion au sharubati zingine ni maarufu sana sehemu hizi za pwani. Leo nimeamua kuwaandalia juice mchanganyiko wa juice ya embe na passion.
Jinsi ya kutengeneza juice ya embe na passion
Vipimo:
Passion fruit 8
Embe 6 za kiasi
Maji kiasi
Sukari kiasi upendavyo
Namna Ya Kutayarisha
1. Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje .
2. Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.
3. Tia sukari korogo ikiwa tayari.
Discover more from Malindians.com
Subscribe to get the latest posts sent to your email.