Home Mapishi Bhajia za Kunde

Bhajia za Kunde

by komzinski
bhajia za kunde zimeiva

Bhajia za kunde ni moja wapo wa aina tofauti za bhajia zinazopikwa mji ya pwani hasa ya Afrika Mashariki. Kama jina linavyoashiria, bhajia za kunde hutengenezwa kutumia kunde zilizosagwa.

Jinsi ya kuandaa na kupika bhajia za kunde

Vipimo
Kunde za kupaaza – 1 ½ Vikombe
Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa – ½ Kikombe
Baking soda – ¼ Kijiko cha chai
*Bizari mchanganyiko – 1 Kijiko cha chai
Maziwa – 2 Vijiko vya supu
Chumvi – 1 ¼ Vijiko vya chai
Unga wa ngano – 2 Vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia
* Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda

Namna ya kutayarisha na kupika bhajia za kunde

 

Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.

Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.

Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.

Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.

Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bhajia.

Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.

bhajia za kunde zimeiva

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More

Privacy & Cookies Policy