Home Entertainment Shampuzi atoka Radio Jahazi

Shampuzi atoka Radio Jahazi

by komzinski
francis shaban shampuzi

Kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja masikio yetu yamezoea sauti ya mtangazaji, Shampuzi katika stesheni mpya kabisa katika mji wa Malindi, Radio Jahazi. Mtangazaji Shampuzi, amewateka wasikizaji hasa masaa ya jioni.

francis shaban shampuzi

Mtandao wa malindians.com umepata habari kuhusu kuondoka kwake kwenye kituo hicho. Hivi ndivyo interview yetu na mtangazaji huyo ilivyoenda:

Malindians: Nakujua kama Shaban Shampuzi, yametoka wapi hayo majina?
Shampuzi: Shaaban Francis ni jina langu rasmi. Shampuzi limetokana na jina nililoanzia “Shaaban jamaa la upuzi “Hii ni baada ya kuwa na majina chungu nzima niliyokuwa nikitumia katika industry.

Malindians:Tuambie kuhusu kazi na taaluma:
Shampuzi: Nilianzia East Africa Institute of Certified Studies ambapo nilifanya diploma ya Mass Communication and Journalism kumalizia 2018. Already nimefanya kazi sehemu tofauti kama ETv, EATV, lulufm ndio nikafika jahazi.

Malindians: umekaa kwa kipindi kifupi Jahazi.
Shampuzi: si kipindi kifupi, nilianza kazi mwaka jana February. So kwa jumla nimemaliza mwaka mzima.

Malindians: so mbona unatoka na kutafuta “greener pastures”?
Shampuzi: Nahisi industry ya media bado iko chini. Na hata kama ina grow, ina grow at a very slow pace. Watu bado hawajatambua umuhimu wa media.

Malindians: mumetokana kivipi, au ni pesa ndio shida?
Shampuzi: Tumeachana na Radio Jahazi vizuri sana. Industry ya Malindi haijaweza kulipa vizuri. Nataka kuangalia bahati yangu Nairobi. Kule mambo yamefunguka vizuri.

Malindians: Tuambie kuhusu wakati uliofanya na Radio jahazi
Shampuzi: Nimejifunza mengi, na nimepatana na watu wa tajriba tofauti tofauti. Hasa nimejifunza uvumilivu na namna ya kukaa na watu. Nimejifunza kuinteract na mafans na watu ambao sikudhania ningepatana nao.

Malindians: Your best moments
Shampuzi: Akifikiria: Nafikiria nikiwa na P3 sauti ya dhahabu (Omar Ngowa) tukifanya kipindi cha jioni cha Kijiweni Drive kila siku kuanzia saa kumi hadi saa mbili usiku. Tulikuwa na chemistry nzuri sana na mwenzangu. Pia mafans wetu wamekuwa pamoja sana na sisi hasa wakati wa gumzo huru kiasi cha kwamba muda huwa unaisha bila ya kutambua kabisa.

Malindians: Changamoto hazikosekani katika kila industry…
Shampuzi: Kazi inahitaji kuwa mbunifu sana. So wakati mwengine ilikuwa changamoto hasa pale ninapokuwa mgonjwa. Hii yote inawezekana unapofanya research ya hali ya juu kabisa.

Malindians: Unawaambia nini mashabiki wako?
Shampuzi: Ningewashukuru sana kwa kunipa fursa na support kwa kipindi nilipokuwa Jahazi. Ninachoahidi kuwa watarajie mambo makubwa kutoka kwangu na sitawaangusha.

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More

Privacy & Cookies Policy