Celebrity Saturday at Stardust Malindi

0
790
celebrity saturday

Celebrity Saturday ni tamasha ambalo linaandaliwa kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi. Ni tamasha ambalo linajumuisha kazi tofauti tofauti za wasanii tofauti tofauti. Sanaa ni moja wapo wa vitu muhimu katika kila jamii. Msanii ni kioo cha jamii na hapa jamii inapata fursa ya kujua, kutambua na kujifunza mengi. Pindi tu jamii inapoweza kuiinua sanaa basi hapo ndipo jamii inapoinuka zaidi.

Celebrity Saturday #1

 

Kama show ya Kwanza ya tamasha hili, Wake Up Tv ikishirikiana na majumba kadhaa ya muziki mjini Malindi ikiwemo Beast Mode Gang inayomilikiwa na msanii Kevin Mode almaarufu K-Mode waliweza kufanikisha tamasha hili ambalo liliandaliwa ndani ya Stardust, club tajika katika mji huu.

malindi nightlife
Bar ya vinywaji ndani ya Stardust

Wasanii walifika kwa wingi na kuweza kuwatumbuiza mashabiki waliokuwa wakingoja kwa hamu. Baadhi ya wasanii walioweza kufika walikuwemo crew nzima ya Beast Mode Gang; K-Mode, Reed Mallis, Khally weedy na Yung Sleazo; Monster Monk, Dee Ommy, Dowg Guerilla, Rued Eye, Lil Mizze na Opty Monsta na wengi zaidi.

Celebrity Saturday #1

Cheki hali ilivyokuwa katika tamasha hilo. Picha zote ziko ndani ya link