Home Burudani Passion AYK

Passion AYK

by komzinski
Passion AYK Music

Passion ama “Passion AYK” kama alivyokuwa akijulikana kipindi cha nyuma ni msanii na producer wa mziki wa mtindo wa hiphop na RnB. Passion mkaazi wa mji wa Malindi, kulingana wa kumbukumbu za serikali, anafahamika kama Felix Onyango Ondeji.

Passion AYK 4 Malindians.com

Passion amekuwa katika sanaa ya kuimba kwa kipindi kisichopungua miaka kumi (10). Anadai kuwa sanaa ya kuimba ilimtafuta yeye bali si yeye kuitafuta kwani ipo kwenye damu. Mzee wake (Baba yake), alikuwa msanii kwa kipindi kirefu, na Passion alikuwa katika mazingira ya sanaa. alijifunza mengi na kila kuchao alifanya mazoezi ya kuimba kutumia nyimbo na mashairi ya wanamziki tofauti tofauti.

Ushauri wa marafiki juu ya kipaji na uwezo wake wa kuimba pamoja na kupatana na Producer Sango katika Black Legend ndio ilikuwa mwanzo rasmi wa safari yake katika ulingo wa sanaa ya kuimba. Katika Black Legend anakumbuka kuwepo kwa wasanii kadhaa akiwemo Young Njita na Bozen AYK.

Passion AYK 8 Malindians.com

 

Kazi alizofanya Passion

Katika kuimba, amefanya kazi kadhaa kama solo artist na pia nyengine nyingi akiwa katika kikundi kinachojulikana kama AYK, Awamu Ya Kwanza. Katika kikundi hichi alijumuisha Bozen AYK na Kalido AYK ikiwa kazi zao zikitengenezwa na Producer Sango.

  1. After
  2. Riziki Passion & Bozen
  3. Yolo – Passion Kalidoh

Changamoto Katika Sanaa

Anadai Sanaa iko na changamoto nyingi sana. Hasa pale msanii anapokosa support ya mshabiki wake. Kwani si kila muda anaweza kutoa ngoma zinazoambatana na matakwa ya mashabiki. Hasa sanaa inaweza kwenda hatua kadhaa iwapo “mapromoter” wataingilia kati na kupiga jeki sanaa kwani si wasanii wote wenye hela ya kusukuma mziki wao inavyotakikana.

Passion AYK 5 Malindians.com

Kwa wamashibiki wake anaahidi mambo makubwa, vitu vikwali vina tayarisha na ni matarajio yake kuwa pindi tu kazi hizo vitapakuliwa kwa mitandao, watakuwa tayari kuzipokea. Kwa vijana wenye vipaji anawapa changamoto ya kutia bidii kwani Waswahili wamesema:

“Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu”

Sanaa kama jambo lengine lolote lile inataka mapenzi, kujituma na kujitolea. Kila umapozidisha mapenzi ndipo mambo yanaponyooka zaidi.

 

You may also like

Leave a Comment

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More

Privacy & Cookies Policy