Zebra cake ni cake iliyobandika jina ya Punda milia kulingana na rangi yake ya weupe na weusi. Upishi huu wa Zebra Cake utaonyesha maana ya kutengeneza aina hii ya keki kuwa tamu na yenye kuvutia kulingana na style ya watu wa Malindi

 

Zebra Cake - Upishi wa Watu wa MalindiJINSI YA KUANDAA ZEBRA CAKE NYUMBANI

Mahitaji

1)sukari (granulated sugar) 1cup

2) mayai 4

3)maziwa kikombe 1

4)mafuta ya kupikia(vegetable,corn au canola) kikombe 1

5)unga wa ngano 2 cups

6)1/3 vanilla ya unga au arki ya vanilla

7)dark cocoa powder 2 tablespoon

8)baking powder 1 tablespoon.

Namna ya kutayarisha

1)changanya sukari na mayai..tumia electric hand mixer au whisk beat kuchanganyia..hadi mchanganyiko uwe laini

2)weka maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri

3)katika bakuli jengine changanya baking powder,vanilla powder na unga pamoja

4)weka huo unga kwenye mchanganyiko wako wa mayai na sukari…changanya

5)gawanya mchanganyiko sehemu 2 sawa

6)sehemu moja iweke pembeni na nyengine weka cocoa yako na uichanganye vizuri.. 7)mimina kwenye trey vijiko 3 vya mchanganyiko plain then weka vijiko 3 vya mchanganyiko wa cocoa…fanya hivo hadi imalizike…(usisubirie mchanganyiko usambae). 8)weka moto 300-350° hadi iwive vizuri

Summary
recipe image
Recipe Name
Zebra Cake
Author Name
Published On