Wali wa nazi na ndimu

Description

VIPIMO:

Mafuta ya nazi kijiko 1 chai
Mchele kikombe 1
Tui la nazi vikombe 2
Ganda la ndimu 1 lilokunwa
Maji ya kipande cha ndimu
Chumvi kiasi

MAELEKEZO:

1. Katika sufuria juu ya moto wa kiasi, kaanga mchele wako kwa mafuta ya nazi kijiko 1 cha chai, kaanga kwa dakika 1

2. Mimina tui la nazi,tia chumvi ya kutoshea kisha koroga vizuri acha uanze kuchemkia, Funikia kwa mfuniko kisha punguza moto uwe mdogi mdogo.

3. Acha wali utokote ukiwa umeufunika kwa muda wa dk 35 au hadi upate kuiva na kukaukia vizuri. Epua kisha acha upoe kidogo kam muda wa dk 10.

4. Funua mfuniko kisha uchambue wali wako taratibu kwa uma, kisha tia ganda la ndimu na maji ya ndimu changanya vizuri. Kula ukiwa moto moto. Enjoy