Wali wa kukaanga na mayai

Description

Vipimo:

Wali ulopikwa vikombe 5
Mayai 3 + mayai 2
Paprika ¼ kijiko cha chai
Manjano ¼ kijiko cha chai
Mafuta vijiko 2 + kijiko 1 chakula
Kitunguu maji 1 cha size kilichokatwa katwa
Hoho nyekundu zilizokatwa katwa ½ kikombe
Njegere zilizoganda na kuacha zikayeyuka 1/2 kikombe
Chumvi kiasi
Sukari ¼ kijiko cha chai
Pilipili manga ¼ kijiko cha chai
Vitunguu vya kijani 2 vilivyokatwa katwa

MAELEKEZO:
1. Kama unatumia wali ulopika wakati huo uchambue vizuri na uma kisha utie katika sahani au Sinia pana acha upoe kabisa, na Kama unatumia ulobaki katika fridge uuchambue vizuri kwa mikono misafi kuuvunja vunja.
2. Piga mayai 3 katika bakuli moja, kisha piga mayai 2 pamoja na maji vijiko 2 chakula, paprika na manjano kisha ziweke pembeni bakuli zako zote mbili.
3. Tia karai au pan jikoni juu ya moto wa kiasi, kisha tia mafuta ya kula vijiko 2 chakula, yakipata moto tia mayai 3 uloyapiga bila viungo