Vitumbua kama kitafunio mitaa ya Uswahilini

Siwezi kumbuka chimbuko la vitumbua kama kitafunio mbali kutoka utotoni nakumbuka  kuwepo kwa vitumbua nikiwa mitaa fulani mjini Malindi. Kitumbua kwa mtu mgeni uswazi ni kitafunio kinachoandaliwa na chai au kuliwa kilivyo.

Kimetengenezwa na mchele uliosagwa na kutiwa ndani yake tui la nazi pamoja na sukari. Mchanganyiko huu unachomwa ndio kupatikana vitumbua.

Upishi wake hubadilika kulingana na mapishi ya watu mbali mbali. Hii pia ni njia moja wapo katika ukurasa wa LifeinMombasa

Mahitaji:-
⚫Mchele wa (vip) vikombe 2
⚫Hamira kjk 1 chai
⚫Tui la nazi kikombe 1
⚫Ute wa mayai 2 (ukipenda)
⚫Sukari kikombe 1
⚫Unga wa ngano kjk 1 chakula
⚫Hiriki kjk 1 chai

MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA.
1. Loweka mchele katika maji usiku mzima.

2. Chuja maji yote kisha utie mchele katika blender pamoja na tui la nazi,unga wa ngano,hiriki na hamira.

3. Saga hadi uwe laini. Mimina katika bakuli,funikia acha sehemu yenye joto ufure hadi ujae mara mbili.

4. Tia sukari na ute wa yai koroga vizuri kuchangananya. Choma vitumbua vyako katika moto wa kiasi hadi vipate rangi ya brown pande zote 2. Enjoy!

Note:-
Kama uji ni mvito sana ongeza maziwa au tui la nazi.

Vitumbua upishi wa Malindi

Recipes & Pic by: Mapishi Mix

Summary
recipe image
Recipe Name
Vitumbua
Author Name
Published On
Total Time
Average Rating
3.51star1star1star1stargray Based on 3 Review(s)