Vitumbua Keki

Description

VIPIMO:-
Unga wa ngano kikombe 1 1/2
Baking powder vijiko 3 1/2 chai
Chumvi Kijiko 1 kasoro chai
Sukari kijiko 1 chakula
Maziwa kikombe 1 + kijiko 1 cha chakula
Kiini cha yai 1
Vanilla kijiko 1 chai
Siagi iloyeyushwa vijiko 3 chakula
Ute wa yai 1
Chocolate chip ndogo ndogo 1/2 kikombe

MAELEKEZO:-
1. Washa oven joto 190°C. Paka chuma chako cha vitumbua mafuta. Weka pembeni

2. Katika bakuli kubwa tia unga,baking powder,chumvi na sukari kisha koroga vizuri kuchanganya.

3. Tia maziwa,kiini cha yai, vanilla na siagi iloyeyushwa. Koroga vizuri kuchanganya ,usiukoroge kwa muda mrefu.

4. Katika bakuli nyingine piga ute wa yai hadi uwe mzito na mweupe, taratibu utie katika mchanganyiko wako wa unga kuchanganya.

5. Tia chocolate chips kama utatumia ,changanya vizuri kisha chota unga wako kwa kijiko au kichotea Icecream(ice cream scopper) kisha jaza katika vishimo vya chuma chako cha vitumbua.

6. Oka kwa dk 12 au hadi ukichoma kijiti Kati kitoke safi.

7. Haraka viweke vitumbua vyako katika wire ili vipate kupoa kidogo.

8. Vitumbua hivi huliwa kwa asali ,marple syrup na rojo/shira mbalimbali za matunda. Enjoy!

NOTE:
Unaweza kuongeza radha kulingana NA taste yako kama vile ukatia ganda la limao,chungwa na arki mbali mbali