Mapishi ya sambusa au samosa kama baadhi ya watu wanavyoita yametajwa kuanzia enzi za karne ya 13 na 14 katika hadithi na ngano za wasafari waliofanya biashara Bara ya Asia. Mtu tajika aliyezungumzia sambusa ni Abolfazl Beyhaqi (995-1077).

Siwezi sema ni miaka gani sambusa zilianza Africa Mashariki ila najua zilikuja na wasafiri wa meli kutoka Bara Arabu na Asia. Mapishi yakaenda na kubandilika kila kukicha. Mapishi ya Sambusa za nyama ya kuku yana kivutio kikubwa kwa watu wanaopenda kula kuku.

sambusa za nyama ya kuku

Jinsi ya kutayarisha Sambusa za nyama ya Kuku

VIPIMO

Manda ya sambusa ya tayari Kiasi inavyouzwa (Kiasi ya sambusa 40-50)

Mafuta ya kukaangia Kiasi

Kuku (kidari) kilichosagwa

1 Kilo Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa

1 kijiko cha chai Pilipili mbichi iliyosagwa

1 Kijiko cha chai Pilipili manga

1 kijiko cha supu Bizari ya pilau ya unga (cummin powder)

1 kijiko cha chai Bizari ya mchuzi

1 kijiko cha chai Ndimu

1 kijiko cha supu Mboga mchanganyiko

1 kikombe Chumvi Kiasi

Nyanya iliyokatwa ndogo ndogo

1 Vitunguu maji vilivyokatwa (chopped)

Namna ya kutayarisha na Sambusa

1. Pika nyama ya kuku ya kusagwa kwa kutia chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, ndimu na bizari zote.

2. Karibu na kuwiva tia mboga za mchanganyiko (frozen vegetables).

3. Zima moto na tia nyanya, vitunguu na kotmiri.

4. Funga sambusa katika mandakama kawaida.

5. Pika sambusa katika mafuta ya moto hadi ziwe nyekundu na zikiwa tayari kuliwa