Sambusa za nyama

Description

VIPIMO VYA NYAMA:

Nyama ya steak ilosagwa ½ kilo
Mchanganyiko wa tangawizi na saumu ulosagwa kijiko 1 chakula
Pilipili manga kijiko 1 ½ chakula
Binzari nyembamba ya unga kijiko 1 chakula
Chumvi kiasi
Maji ya limao kijiko 1 chai

VIPIMO VINGINE:

Vitunguu maji 2 vilivyokatwa shape ya vibox
Karoti zilizokunwa ½ kikombe
Majani ya giligilani yalokatwa katwa ½ kikombe cups
Giligilani ya unga kijiko 1 chai
Binzari nyembamba ya unga kijiko 1 chai
Manjano 1/2 kijiko chai
Pilipili nyeupe kijiko 1 chai

NAMNA YA KUTAYARISHA:

1. Changanya mahitaji yote ya nyama katika bakuli, funikia acha viungo viingie kwa muda wa nusu saa.
2. Chemsha nyama yako hadi iive , kisha epua.
3. Tia mafuta ya kula ktk sufuria jikoni, moto uwe wa kiasi, yakipata moto tia vitunguu kisha kaanga hadi vilainike ila visibadili rangi.
4. Tia karoti ulizokunwa pamoja na viungo vyote,kaanga kwa sekunde 1 kisha tia nyama ilowiva, kaanga kwa dk 2 hadi ijichanganye vizuri na viungo. Epua acha ipoe kidogo.
5. Jaza nyama yako katika manda za sambusa,funga vizuri kisha kaanga ktk moto wa kiasi hadi zipate rangi ya brown... Enjoy !

Note:-
Unaweza chemsha nyama steak isosagwa kisha baada ya kuiva ukaisaga pia.. Hakikisha unanunua nyama isiyokuwa na mishipi wala mafuta ,nunua nyama fresh kisha wakusagie, usinunue ilosagwa kabisa inakuwa haina ubora