Pilau ya Maharagwe

Description

Pilau ni mojawapo wa vyakula maarufu sio pwani ya Kenya tu mbali pia pwani ya Afrika Mashariki nzima. Jifunze kupika Pilau ya Maharagwe leo

VIPIMO:

Mafuta ya kula vijiko 2 chakula
Bizari nyembamba (cumin) kjk 1 chai
Tangawizi ilokunwa kjk 1 chakula
Nyanya 3
Maharage mekundu yalopikwa kikombe 1
Binzari nyembamba ya unga kjk 1 chai
Giligilani ya unga kijiko 1 chai
Chumvi kijiko 1 chai
Sukari kijiko 1 chai
Mchele wa basmati ulolowekwa dk 15, kikombe 1
Madalasini kijiti 1
Karafuu 3
iliki 2
Ndimu/limao 1
Majani ya giligilani yalokatwa katwa kiasi (kupambia)

NAMNA YA KUPIKA

1. Tia sufuria na mafuta jikoni, yakipata moto tia binzari nzima acha zianze kutokota kisha tia tangawizi na kaanga kidogo.
2. Tia nyanya kisha zikaange hadi zipate kulainika.
3. Tia maharage, binzari ya unga na giligilani ya unga kisha koroga vizuri kuchanganya.
4. Tia chumvi, sukari pamoja na Maji kikombe 1 acha yachemkie katika moto wa kiasi kwa dk 10.
5. Tia mchele na maji tena kikombe 1, tupia viungo vizima koroga vzr kisha funikia.
6. Punguza moto kisha acha uchemkie taratibu hadi wali uive na kukaukia vizuri.
7. Zima jiko kisha acha wale ukae kwa dk 5-10.
8. Kamulia ndimu juu ya wali wako kisha tupia majani ya gigilani...uchambue wali wako kwa uma. Kula ukiwa moto kwa salad ya mtindi. Enjoy!