Mikate ya Maji ya Nutella

Description

VIPIMO:
Unga wa cake kikombe 1
Maziwa kikombe 1
Maji ½ kikombe
Sukari ¼ kikombe
Yai 1
Chumvi 1/4 kijiko chai
Mafuta ya kula kwa ajili ya kupakaza chuma
Nutella kwa ajili ya kujaza
Chocolate ya nutella iloyeyushwa (ukipenda)

MAELEKEZO:-

1. Katika bakuli ya kati tia Mahitaji yote kisha piga hadi mchanganyiko uwe smooth.

2. Tia chuma chako ulichokipaka mafuta jikoni katika moto wa kiasi.

4. Mimina unga wako wa mikate ya maji ktk chuma chako,chota 1/4 kikombe ya unga kwa kila mkate.

5. Zungusha chuma chako kueneza unga wako na kufanya duara.

6. Pika mkate wako kwa sekunde 30 au hadi chini ipate rangi.

7. Geuza upande wa pili kwa kutumia spatula kisha acha na upande wa pili upate kuiva,epua ktk sahani, Rudia kumaliza unga wote.

8. Paka Nutella juu ya mkate wako isiwe nyingi sana kisha zungusha kama picha inavyoonyesha. Utarudia kwa zote

9. Pambia kwa kunyunyiza chocolate uloyeyusha (ukipenda)

Note:
Unga wa crepe au mikate ya Maji hasa unayojaza inatakiwa uwe mwepesi zaidi