Cheki maandalizi na upishi wa mboga ya mchicha. Mapishi yapo mengi lakini mapishi haya ya mboga hii kama wanavyotayarisha watu wa Malindi yatakupendeza na kukuvutia mno. Pia unaweza kuangalia upishi wa mboga ya mchicha na matumbo

recipes ya mboga ya mchichaJINSI YA KUANDAA NA KUPIKA MBOGA YA MCHICHA

Mahitaji:

1,Mchicha (Kiasi kinachokutosha).

2.Kitunguu maji.

3.Nazi ( tui zito/ ya pakiti).

4.Curry powder.

5.Pilipili (ukipenda).

6.Mafuta ya kupikia kiasi.

7. Karoti. chumvi

Jinsi ya kuandaa:

1.Chambua mchicha wako, uoshe vizuri weka pembeni uchuje maji ( unaweza kuukata kata ukipenda).

2.Weka sufuria jikoni, tia mafuta kiasi, yakipata moto tia vitunguu maji.

3.Kaanga vitunguu, vikiaribia kuwa rangi ya kahawia, weka pilipili nzima, kaanga pamoja na vitunguu.

4.Kisha weka curry powder pamoja na mchicha. 5.Mchicha ukianza kulainika weka tui la Nazi. .changanya vizuri tui na mchicha.

6.Tia chumvi, acha mpaka tui likaukie na uepue mchicha wako tayari kwa kuliwa.

NB; Usifunike sufuria katika hatua zote hizo ( kufunika mboga ya majani kunaifanya itoe maji mengi)

Mboga hii inaweza kuliwa kwa ugali au wali.