Kaimat za Shira

Description

VIPIMO:

Unga wa ngano 1/2 kilo
Samli kikombe cha kahawa
Hamira vijiko 2 1/4 chai
Hiriki kiasi
Ndimu 1
Maziwa kikombe 11/2 -2

NAMNA YA KUPIKA
1. Tia samli katika sufuria ipate moto.
2. Tia unga katika bakuli kisha mwagia samli ya moto kisha fikicha hadi ujichanganye vizuri na upoe.
3. Tia mahitaji yalobaki kisha upige vizuri kwa mkono hadi usiwe na mabonge na uwe tepe was kuvutika. Acha uumuke ukiwa umeufunika.

VIPIMO VYA SHIRA

Sukari kilo 1
Ndimu 1
Arki ya rose kijiko 1 (ukipenda)
Arki ya machungwa kijiko 1
Maji vikombe 2

NAMNA YA KUTAYARISHA.

1. Changanya mahitaji yote katika sufuria, tia jikoni acha ichemkie hadi sukari owe nzito.
2. Kamulia Maji ya ndimu unga wako uloumuka kisha piga tens kidogo kuchanganya.
3. Tia mafuta jikoni ktk moto was kiasi yakipata moto chota unga wako kwa vidole kufanya viduara kisha dondosha ktk mafuta ya moto.
4. Kaanga ukiwa wageuza geuza hadi zipate rangi ya brown.
5. Epua kisha tia katika shira ienee vzr,Rudia kumaliza unga wote.. Enjoy!

Recipe by Mapishi Mix