Pilka pilka zangu hunipeleka sehemu nyingi na kwa bahati nzuri nimepatana na watu wengi wa hulka tofauti tofauti. jana nilikuwa katika show ya karaoke ndani ya Pine court beach bar. Wiki hii, msanii kwa kufoka na Kuimba Kelsa Kelvin alikuwa “Guest Artist”. Nilipatana na Kijana mtanashati kwa jina William Karisa aka kabyser. Hivi ndivyo mazungumzo yalivyoenda:-

willy K

Komz: Nimependezwa unavyoimba, je wewe ni Msanii?
Willy K: Tukifafanua Msanii kwa lugha za kisasa, Mimi si Msanii. lakini nimehusika kwa sana katika kazi za sanaa.

Komz: Wamaanisha nini?
Willy K: nimeshaandika mistari kadhaa lakini bafo sijaingia ndani ya studio na kurecord.
imekuaje kuaje Leo umeamua kuingia mzima mzima katika sanaa?
(huku akitabasamu) Leo nimekuja kumpa backup mdogo Wangu (akiashiria Kelsa).

Komz: Inakuaje mdogo wako ameingia katika Game lakini wewe umechelea?
Willy K: Miaka ya nyuma ilikuwa migumu na wazazi walikataa kuelewa muziki kama kazi. lakini kila kukicha mawazo Yao yamekuwa yakibadilika.

Komz: umezungumza kuhusu kuandika mistari, hebu nimeleze….

Willy K: Yap, nimeandika nyimbo mbili za gospel, Lau ningepata nafasi mapema ningebeba CD za hizo nyimbo.

Komz: je unapanga kurecord nyimbo yako hivi karibuni?
Willy K: Ninapanga kuandika na kurelease nyimbo nikimshirikisha mdogo Wangu Kelsa….

Huenda wazazi walichangia Willy K asifuatilie kipaji chake cha mziki hapo awali, lkini ako na ari ya kufuatilia mziki hivi sasa. Funzo nililopata ni kuwa upatapo fursa ya kufuatilia ndoto, usiiache.