Nimekuwa supporter wa mziki wa humu nchini hasa mziki wa pwani (Malindi kwa sana) na nimejaribu kutumuia mbinu tofauti kujaibu kuupeleka level mbele. Kama blogger humu pwani, kuna changamoto nyingi sana. Wakati mwingi tunawekwa pahali pagumu. Wazungu wanapaita “between a rock and a hard place”.

uchoyo uchoyo uchoyo uchoyo

Mambo mengi mabaya yanafanyika katika jamii yetu lakini sisi tunafaa kubakia kimya kwa sababu inaonekana ndio tutaharibu. La sivyo, sisi ni vioo vya Jamii na inatubidi tuseme la sivyo kutaendelea kuharibika.

Nimecheki video moja ya msanii Chipukizi Dazla akimshirikisha dada Sis P. Video hii ni maajabu matupu. Beat ya nyimbo hio ni nzuri, utunzi mzuri na hata sauti nzuri, lakini video hio inaleta maswali mengi kuhusu maadili ya mwanamuzuki na wanaotengeza video hizi. Je hizi ni kiki pia au kuushiwa na mawazo.

Najua kuna video mbaya zaidi ambazo wahusika wamevaa vibaya zaidi lakini sisi kama wapwani umebakia mstari wa mbele kudumisha maadili mema.

Anyway, lazima tuseme sitabakia kusema langu jicho kwani mwengine ataiga na atasema inakubalika kwa Produza Khalid ashafanya na hamukusema lolote.

Je, unadhani “team mafisi ” ni wa kulaumiwa?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here