Toleo la pili la Malindi Town Art Extravangaza ilifanyika hapo jana (1st August 2015) Maeneo ya Malindi Marine Park kuanzia Saa Tisa Mchana Hadi Saa mbili usiku. Kwa sababu ambazo sikuweza kuziepuka, sikupata nafasi ya kwenda mapema, lakini mida ya saa tatu usiku, nilitoka maskani na machizi wangu kadhaa na kuelekea Marine Park ambapo show  ilikuwa inafaa kuendelea hadi saa sita usiku. Mara tu nilipofika, nilipata giza kali na Patrol ya nguvu kutoka kwa wasimamizi. Baada ya kuzungumza kwa muda na afande aliyekuwa area, ilibainika kuwa shida za mataa ndizo zilizofanya show kusimamishwa mapema.

Nilirudi mtaani na kusubiri kusimuliwa katika mitandao ya kijamii hasa Facebook.

Kulingana na Habari nilizozipata kwa account ya David ‘D-boy’ Evance na Marvin Brudas ni kuwa show ilifana sana. Hii ni hatua kubwa sana kama wakazi wa malindi tulio weza kupiga.

Habari zinazojitokeza sasa ni kuwa show iliyokukusudiwa kuwa nafasi ya kuonyesha talanta kwa wasanii wa Malindi town ilitekwa na wasanii kadhaa hasa wale wanajuana na walioandaa Extravangaza hii.

Hii ni baada ya kuona matamshi makali ya msanii Rued Eye katika mtandao wa Facebook.

beef

Rued Eye akipata Backup kutoka kwa Dowg Guerrila anadai kuwa Young Njita and Malindi records wanakanyagia vipaji mjini Malindi. Kulingana na Rued Eye, hawa wawili (Young Njita and Malindi records) waliwabania wasanii wengine kuperform kwa show hiyo.

Wakati nikiandika story hii, sijapata nafasi kuongea na wahusika wa pande mbili ya hii story. Lakini nitafanya juu chini ili kujua ukweli

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here