Kulingana na taarifa tulizozipata kwa mitandao kwa kijamii al maarufu Facebook kutoka kwa Ripota Barabarani aka TUKTUK DRIVER 001 aka Kibadi Kipanga ni kuwa kalameni mmoja aliyedai kuwa afisa wa manispaa mjini Malindi kenya alirushiwa tiktak kadhaa wakati alipojaribu kumkamata dereva wa bajaj kwa kigezo cha kuwa alikuwa amevunja sheria za barabara. Inavyosemeka ni kuwa karate, ngumi na mateke ya jamaa huyo yalionyesha wazi kuwa huyu jamaa alikuwa amesomea Tae Kwondo. Jamaa walikusanyika kushuhudia sinema ya bure, tukio ambalo lilikumbusha wananchi kuhusu filamu za Karate na Kungfu za akina Bruce Lee, Jackie Chan na Bolo Yeung.

bajaj-malindians  afisa-malindians

Kulingana na matamshi ya watu katika mtando huo ni kuwa askari wa manispaa wamekuwa na tabia ya kujificha vichochoroni na nguo zisizo sare ya kazi aka “UnderCover” aka “Detectives” na kushika hasa waendeshaji pikipiki aka Bajaj. Oparesheni kama hivi zimekuwa zikienda “Haywire” na kuleta ajali kadhaa. Hivi majuzi oparesheni mmoja ilisababisha hasara kwa biashara ya mama fulani anayejulikana kwa jina la mtani aka nickname kama “Waziri wa Wanaume” wakati Bajaj ilipogonga beseni lake la mitai baada ya mwendeshaji pikipiki kuvamiwa ghalfa na “maafisa wa Special Unit” waliokuwa mafichoni.

Ili kufuatia zaidi mazungumzo hayo, ingia mtandao wa kijamii wa facebook, group ya Malindi Kenya

SHARE
Previous articleMalindians S01E06 – Miles
Next articleMalindians S01E07 – Malindi Rotaract Club
Why have I been traveling so much? Because I have grown to like and love Malindi, I want to take risks, meet interesting people, challenge myself, explore the world, and learn more about myself in the process. This also helps me tell the story of how interesting Malindi.