Kawaida huwa sipendi kugusia mambo yanayoingilia¬†maisha ya watu, hasa maisha ya watu wa uswazi. Lakini leo inanibidi niseme, kwani ni jambo linalokera sana. Nilikuwa katika pilkapilka zangu ukipenda raundi mwenda katika mitaa ya “Kifahari” ya Kisumu Ndogo (kwa sababu ya airport) mjini Malindi, ndipo nilipopata fununu ya yalitendeka asubuhi. Ilikuwa mida ya kiamsha kinywa wakati akina Abdoo (si jina la ukweli) walipokuwa wakinywa chai huku wakisuburi mbuzi walioletwa kichinjioni kununuliwa ¬†walipomuona kalameni huyu aka Mwalimu Mkuu wa Shule ya XXX ¬†(jina limebanwa ) akiandama na mtoto wa asili ya Kisomali (Cushite) kutoka kwa guest mmoja iliyoko karibu na kichinjio hicho. Kama wakereketwa, ilibidi kuingilia kati na kumhoji binti yule kutumia lugha ya mama. Loh!!!! Amini usiamini, Mwalimu mkuu huyo amekuwa akijienjoy full kujiachia si mara ya kwanza au ya pili bali ya tatu. Ghadhabu iliwajaa Abdoo na “wendani” na kuanza kurusha karate mithili ya muigizaji mkongwe wa filamu za ndondi Jackie Chan. Sinema hii ya bure ilivutia umati, watu walijaa teleeee!!! Basi ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Maajabu haya kuishia hapo. Inavyosemekana, Binti huyo alikuwa amekubali kitita cha Shillingi elfu taslimu na alikubali kustarehe na mwalimu huyo hasa vile shule imefungwa. Ilikuwa jambo la kusikitisha kwani ilidhaniwa kuwa binti huyo alikuwa amelazimisha na Mwalimu huyo. Baada ya kuona kibano mithili ya kile angepewa mwenda wazimu aliyeingia msikitini na kubaulia kitabu kitakatifu, reporter wangu alihofia Mwalimu mkuu huyu angepoteza maisha. Kwa hivyo alimpigia simu Koplo (corporal) Mwiti wa Kituo cha Polisi cha Malindi ambaye hakulalia masikio na kufika sehemu hiyo mara moja. Wakati habari hii inaenda hewani, reporter wangu hana habari juu ya hatima ya Mwalimu huyu. Kama kawaida maswali mengi tunabaki kujiuliza:- 1. Je Mwalimu huyu anastahili kupewa jukumu la kuwa kielekezo chema kwa watoto wetu au huu ni mfano wa kumuachia mbweha kuchunja kondoo? 2. Je Mwalimu huyu atafunguliwa mashtaka? Sina uzoefu wa kituo cha polisi, kwa hivyo najaribu kutafuta kama taarifa hii iko katika kitabu cha matukio na ripoti za Polisi (Occurrence Book aka O.B.)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here